Viongozi wa dini mbalimbali kanda ya Kaskazini (Interfaith Forum) wamekutana mkoani Singida tarehe 5.5.2025. Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa dini kutoka mikoa Tanga,Kilimanjaro, Arusha, Manyara, na Singida na ulikuwa na kauli mbiu “UPENDO HAKI NA AMANI “.
Katika mkutano huo Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Askofu Dkt. Fredrick Shoo alitoa wito kwa vyombo vya dola vilivyoko chini ya mamlaka, kuwa na weledi katika kutimiza majukumu yao.
Akizungumza kuhusu vyombo vya dola alisema, mahali pengine imetumika nguvu ya ziada na hata watu wasio na hatia kujeruhiwa, kupigwa na kadhalika. Tunapenda kusema hatupendi kuyaona haya. Tukumbuke viongozi wa dini ndio kimbilio la pekee na la mwisho la kutetea wananchi katika masuala mbalmbali yanayogusa maisha yao kimwili, kiakili na kiroho”. Alisema Askofu Shoo.
Aidha alisisitiza kuwa, tusiruhusu ubaguzi unaozaa chuki na mafarakano, kila mmoja awajibike kwa nafasi yake maana kila mmoja atatoa hesabu ya chochote anachokifanya katika nafasi yake kama kiongozi na kama raia.


