Kuwahudumia Watu Wenye Mahitaji Maalumu ni Wajibu wa Kanisa

Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini amesema, suala la kuwasaidia na kuwahudumia watu wenye mahitaji maalumu ni wajibu wa Kanisa.

Askofu Shoo, aliyasema hayo alipokuwa akigawa viti mwendo kwa watoto wenye ulemavu wa viungo Jimbo la Karatu. Jumla ya viti mwendo 24 vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 1.5 viligawanywa kwa baadhi ya wahitaji katika Jimbo la Karatu Agosti 17, 2024.

Msaada huo umetolewa na Dayosisi ya Kaskazini kupitia Kitengo cha Building a Caring Community (BCC) kilichopo Idara ya Diakonia ya KKKT Dayosisi Kaskazini.