Siku ya Maombi ya Dunia

Siku ya Maombi ya Dunia imefanyika katika Ibada ya asubuhi ofisi Kuu ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini Machi 4, 2022 na kuongozwa na Mch. Faustine Kahwa katibu wa Idara ya Wanawake Dayosisi.

Miongoni mwa mambo yaliyoombewa ni pamoja  na ustawi wa nchi, watu na viumbe wote pamoja na kurejesha mfumo wa asili usio na madhara kwa uumbaji wa Mungu. Pia wameomba amani ya Mungu na ulinzi kwa watu wanaoishi kwa hofu, waliopoteza amani, wenye njaa na taabu mbalimbali.

Mwongozo wa Siku ya Maombi ya Dunia mwaka huu umeandaliwa na kamati ya siku ya maombi ya dunia ya Uingereza, Wales na Ireland ya Kaskazini na kutafsiriwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT)Idara ya Wanawake Watoto na Jinsia na kuhaririwa na Idara ya Wanawake Dayosisi ya Kaskazini.

Neno kuu limetoka kitabu cha Yeremia 29:11 “Mungu anatuwazia mawazo yaliyo mema”

Baadhi ya watumishi wa Ofisi kuu ya Dayosisi ya Kaskazini kwenye picha ya pamoja mara baada ya Ibadaya ya Siku ya Maombi ya Dunia Machi 4, 2022