NAFASI YA KAZI – AFISA MANUNUZI NA UGAVI

NAFASI YA KAZI – AFISA MANUNUZI NA UGAVI

05 Agosti, 2026

  TANGAZO LA KAZI

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) – Dayosisi ya Kaskazini ni taasisi ya dini inayomiliki na kuendesha taasisi mbalimbali za kijamii na kiuchumi. Katika kuimarisha usimamizi wa rasilimali zake Dayosisi inatangaza nafasi ya kazi ya AFISA MANUNUZI NA UGAVI.

 KITUO CHA KAZI: Dayosisi ya Kaskazini –Ofisi Kuu MOSHI

 Lengo la Nafasi

Kusimamia na kuratibu kwa weledi shughuli zote za Manunuzi na Ugavi za Dayosisi, kwa kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za manunuzi .

Majukumu Makuu

  • Kuandaa na kutekeleza mpango mwaka wa manunuzi “Procurement Plan”.
  • Kukusanya taarifa za kusaidia kutayarisha makisio ya vifaa vinavyohitajika.
  • Kuratibu mchakato wa zabuni na uchaguzi wa wazabuni.
  • Kusimamia ununuzi wa bidhaa, vifaa, huduma na kazi mbalimbali za Dayosisi.
  • Kusimamia upokeaji,uhifadhi na ugawaji wa vifaa.
  • Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa bajeti za idara.
  • Kuweka kumbukumbu sahihi za manunuzi na mali za taasisi.
  • Kusimamia utunzaji wa ghala na hati/kumbukumbu ya vifaa vilivyomo ghalani.
  • Kufuatilia mikataba ya manunuzi na kuhakikisha inatekelezwa ipasavyo.
  • Kuandaa taarifa za manunuzi na ugavi na kuziwasilisha kwa uongozi kila mwezi.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na kiongozi wake

Sifa za Mwombaji

  • Shahada ya kwanza au zaidi katika moja ya fani zifuatazo; “Material Management”, “Procurement and Logistics/Management Science” au fani inayohusiana na hizo kutoka chuo kinachotambulika na Serikali.
  • Awe amesajiliwa na “Procurement and Supplies Professionals and Technicians Board “(PSPTB)kwa kiwango kinachostahili.
  • Awe na Uzoefu usiopungua miaka 5 (angalau miaka 2 katika nafasi ya uongozi)
  • Awe Muadilifu na maadili ya Kikristo
  • Umri: miaka 30 – 45

 MSHAHARA NA MARUPURUPU

Mshahara na marupurupu yatatolewa kulingana na muundo wa maendeleo ya utumishi wa Dayosisi ya Kaskazini.

JINSI YA KUTUMA MAOMBI

Waombaji wanatakiwa kuwasilisha:

  • Barua ya maombi
  • Wasifu binafsi (CV)
  • Nakala za vyeti (zilizothibitishwa)
  • Nakala ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
  • Majina na mawasiliano ya wadhamini (referees) wawili.

Barua pepe: ajira@elctnortherndiocese.org (maombi yote yawe PDF)

Yakiwasilishwa kwa:
Katibu Mkuu
KKKT – Dayosisi ya Kaskazini
S.L.P 195, Moshi

Mwisho wa kupokea maombi:  21 Agosti, 2026

 

 

Job Type: Full Time
Job Location: Moshi

Apply for this position

Allowed Type(s): .pdf, .doc, .docx