Siha District

Mkuu wa Jimbo

Mch. Elisa Kileo

Contacts

Phone: 0764 751 670

Mkuu wa Jimbo wastaafu

  1. Mch. Eligard V. Nassari (1987 – 2008)
  2. Mch. Elisante F. Maimu (2008 – 2010)
home-siha

Jimbo la Siha ni moja ya majimbo matano (5) ya Dayosisi ya Kaskazini. Jimbo la Siha lilianza kwa kugawanyika toka lililokuwa Jimbo la Kilimanjaro Magharibi mwaka 1987 likaitwa Jimbo la Hai Magharibi. Mkuu wa jimbo wa kwanza akiwa Mch. Eligard V. Nassari.

Jimbo la Hai Magharibi lilibadilishwa jina lake na kuwa Siha mwaka 2006, mara baada ya eneo la Siha kuwa wilaya kamili na kuitwa kwa jina la Siha.

Jimbo hili lilianza likiwa na sharika 11. Na idadi ya washirika ilikuwa 26,734 (watu wazima 13,291 na watoto 13,443).

Kufikia sasa jimbo lina sharika 21, mitaa 71, na wakristo watu wazima 15,924, watoto 17,544, na jumla yake ni wakristo 33,289. Kwa takwimu za 2010