Karatu District

Mkuu wa Jimbo

Mch. Barikiel Bura Panga

Contacts:

Phone: 0754 879 245
Email: kjimbolakaratu@gmail.com

Wakuu wa Jimbo wastaafu

  1. Mch. Gabriel Q. Bayda
  2. Mch. Yothan Baha
  3. Mch. Israel Y. Natse
  4. Mch. Samweli Slaa Naaman
home

Jimbo la Karatu ni sehemu ya majimbo matano ya Dayosisi ya Kaskazini, lilianzishwa tarehe 27 – 28/09/1972.  Mkuu wa jimbo wa kwanza ni Mch. Gabriel Q. Bayda, alisimikwa katika usharika wa Oldeani mtaa wa Qunis tarehe 04/02/1973. Huduma hii ilifanywa na Mhe. Askofu Dkt. Stephano R. Moshi.

Jimbo la Karatu lina sharika 15 na mitaa 70, kutokana na fomu ya takwimu ya za washarika kwa mwaka 2017 inaonyesha kuwa, jimbo letu lina wakristo watu wazima 12,239 (Wanawake 6,890; wanaume 5,349), na watoto 13,110 (wasichana 7,217; wavulana 5,893). Jimbo lina jumla ya wakristo 25,349 (wanawake 14,107; wanaume 11,242). Kati ya hawa wanafunzi ni 1,465 (ambapo wasichana ni 836 na wanavulana ni 629).

MAHUSIANO
Jimbo letu la Karatu la KKKT Dayosisi ya Kaskazini, kwa muda sasa limekuwa na mahusiano na marafiki mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, Marafiki hao ni pamoja na

  1. Jimbo la Altdorf Ujerumani
  2. Wawezeshaji wa mradi wa chakula kwa watoto wake (Food for His Children Tanzania) toka Marekani
  3. Kids at Heart (Watoto wa moyoni))

Na pia kila usharika katika jimbo letu una usharika rafiki kule Altdorf kama jedwali linavyoonyesha

Huduma

  1. Hospitali ya Kilutheri Karatu (Hospitali teule ya Wilaya ya Karatu)
  2. Chuo cha Afya Karatu
  3. Chuo cha Karatu VTC
  4. Karatu Lutheran Hostel
  5. Shamba la Karatu Lutheran (Estate)