Hai District

Mkuu wa Jimbo

Mchg. Biniel Eliufoo Mallyo

Contacts
Phone: 0745 363 631

hai-slider

Jimbo la Hai ni mojawapo ya Majimbo Matano ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini lililopo katika wilaya tano za kiserikali yaani Hai, Siha, Moshi Meru na Simanjiro. Kwa sehemu kubwa Jimbo linahudumu katika wilaya ya Hai yenye idadi ya watu 210,533, wanaume wakiwa ni 56,500, wanawake ni 154,033, ambapo kuna tarafa 3, kata 14 na vijiji 61. (chanzo ni sensa 2012 – Tanzania).
Jimbo letu limegawanywa katika Kanda 5 zinazoundwa na Sharika 49 zenye Mitaa 116 inayofanya Ibada kila Jumapili na Jumuia 842 zinazokutana kila wiki. Bado kuna Sharika zenye idadi ndogo ya Jumuia ukilinganisha na idadi ya Washarika waliopo.
Jimbo letu lina washarika 92,798 kati yao watoto ni 25,721 (28%) na watu wazima ni 67,076 (72%). Katika watu wazima, Wanaweke ni 37,647 (56%) na Wanaume ni 29,429 (44%).

Taswira na Dhamira:
Jimbo letu ambalo ni sehemu ya Dayosisi ya Kaskazini,’l’aswira yetu ni: `Ushirika wa Wakristo waliobarikiwa, waliojaa furaha, amani, upendo na waishio ndani ya uzima wa milele katika Kristo Yesu.

Dhamira yetu ni:
KKKT Dayosisi ya Kaskazini imejitoa kwa dhati kutangaza, kuhubiri na kufundisha Injili ya Yesu Kristo na kutoa huduma za kijamii kwa jamii yote.

UHUSIANO
Jimbo letu lina uhusiano na jimbo la Roternburg Ujerumani. Uhusiano huu ni wa muda wa takribani miaka 30 sasa. Uhusiano huu umezaa mafanikio mengi kwa pande zote mbili. Kwa upande wa jimbo letu zipo alama nyingi zilizotokana na uwepo wa uhusiano huu, mfano mzuri ni HVTC, kituo cha mafunzo ya kilimo Boloti n.k. Hivi karibuni tumeanzisha uhusiano na jimbo la Forchhiem Ujerumani ambapo kwa sasa wana mradi wa kujenga chuo cha ufundi usharika wa Sawe.

HUDUMA ZITOLEWAZO NA JIMBO LA HAI

SHULE ZA SEKONDARI

  1. SHULE YA SEKONDARI BOLOTI
  2. SHULE YA SEKONDARI UROKI
  3. SHULE YA SEKONDARI MASAMA
  4. SHULE YA SEKONDARI MSUFINI
  5. SHULE YA SEKONDARI NRONGA

VYUO VYA UFUNDI

  1. URAA VTC
  2. CHUO CHA UFUNDI HAI
  3. SAWE VTC

SHULE ZA MSINGI MFUMO WA KIINGEREZA EMS

  1. MASAMA EMS
  2. MARTIN RUSEL
  3. KUSIRIEU EMS

HOSPITALI

  1. HOSPITALI YA MACHAME