Wahitimu 125 wa kidato cha nne wa Agape Junior Seminary wamehitimu masomo yao kwenye mahafali ya 26 na kupewa vyeti vyao ‘Living Certificate’ na mgeni rasmi Askofu Dkt. Spirian Hillint wa KKKT Dayosisi ya Kati Novemba 26, 2022. Mahafali hayo yaliongozwa na Msaidizi wa Askofu Dayosisi ya Kaskazini ambaye ni mwenyekiti wa Bodi ya Agape Juniour Seminary Mch. Deogratius Msanya.
Kabla ya zoezi la Ugawaji wa vyeti, Mkuu wa Seminary ya Agape Mch. Rodrick Limo alisema jumla ya wahitimu 125 watafanya mitihani yao ya mwisho ambapo alisema wameaandaliwa vyema katika mitihani yao ya mwisho.
Alisema, malengo ya seminari hiyo ni pamoja na kuandaa wanafunzi kuwa viongozi waadilifu wenye kumcha Mungu wakiwa na elimu bora. “Lengo letu ni kuwaanda wataalamu bora wenye maadili mema, wanaomcha Mungu watakaolitumikia kanisa, taifa na dunia”. Alisema Mch. Limo.
Kuhusu taaluma shuleni hapo, mkuu huyo alisema maendeleo kitaaluma yamekuwa mazuri kwa kuwa na ufauli mzuri wa daraja la kwanza na la pili pekee pasipo kuwa na daraja la tatu na waliofeli.
Anasema kwa mwaka jana kidato cha pili kati ya wanafunzi 150 waliofanya mitihani ya taifa, wanafunzi 127 walipata daraja la kwanza, 123 walipata daraja la 2 na hakuna alyepata daraja la 3, la 4 wala aliyefeli.
Anaeleza rekodi ya kidato cha nne mwaka 2021 ilikuwa kati ya wanafunzi 94 wanafunzi 59 walipata daraja la kwanza ni 35 na daraja la pili na hakuna aliyepata daraja la tatu wala aliyefeli. Hali kadhalika kwa kidato cha sita wamefaulu kwa daraaja la kwanza na la pili tuu kwa mwaka 2022.
Vile vile Mch. Limo alisema kuwa, Shule ya Seminary Agape katika mitihani ya taifa mwaka 2021 ilishika nafasi ya 27 kitaifa kati ya shule 644, nafasi ya 3 kimkoa kati ya shule 51 na nafasi ya 1 kiwilaya.
Mkuu huyo alitoa wito kwa wazazi, walezi, serikali na jamii kwa ujumla kushirikiana kwa pamoja katika kuwalea watoto na vijana kuwa na maadili na mazuri. “Wazazi na walezi tutenge muda wa kutosha kuwaelimish na kuwaelekeza watoto na vijana.
Aliwataka wanafunzi hao kudumisha uadilifu na yale yote waliyofundishwa shuleni hapo. Anasema mbali na masomo ya darasani wahitimu hao wamefundishwa kufanya kazi mbalimbali za mikono kama kilimo na.stadi za maisha.
“Pia Wanafunzi wetu wameandaliwa.vyema kiroho kwa kushiriki shughuli zote za kiroho katika seminari yetu kama Bible study, kuongoza ibada, kushiriki semina za neno la Mungu na kujifunza muziki”. Alisema Mchungaji Limo.
Naye mgeni rasmi katika mahafali hayo Askofu Dkt. Spyrian Hilint alipongeza Dayosisi ya Kaskazini kwa mchango wake katika huduma mbalimbali za kijamii hapa nchini. Alisema Dayosisi imeonyeaha kwa vitendo katika kutoa huduma kwa taifa, jamii na kwa watu binafsi kwa kiwango kikubwa.
Aidha aliwaasa wahitimu kuishi kwa kuzingatia maadili waliyofundishwa wakimshika Mungu. Alisema illi ndege aruke vizuri anahitaji mabawa 2, akimaanisha wanahitaji elimu na Mungu, akili na maadili.
Dkt. Hilinti anasema Mungu ni nguvu ya maisha hivyo wanapaswa kuwa na maarifa pamoja na neno la Mungu. Anasema katika maisha inafaa kuzingatia elimu, ibada, tabia njema na neno la Mungu.
Shule ya Sekondari agape kwa sasa ina.wanafunzi 579 kidato.cha kwanza.hadi cha 6 na inamilikiwa na KKKT Dayosisi ya Kaskazini.
