Nkwansira: Usharika wazinduliwa, Ofisi, nyumba ya Mchungaji vyazinduliwa, Wapya waingizwa kazini, Wastafishwa waliomaliza muda wao

Jumapili ya tarehe 28.11.2021 Baba Askofu Dr Fredrick Onael Shoo aliongoza Ibada yenye matendo matano katika Usharika wa Nkwansira Jimbo la Hai. Moja alizindua rasmi Usharika wa Nkwansira, pili alifungua ofisi ya Usharika, tatu alizindua nyumba ya Mchungaji nne aliwaingiza kazini viongozi mbalimbali wa Usharika na tano kuwaaga wazee waliomaliza muda wao.

 Mahubiri yalitoka katika kitabu cha Mathayo 24:42-44 ambapo Mhe. Msaidizi wa Askofu Mch Deogratius Msanya alihubiri. Kichwa cha somo kinasema Bwana analijia Kanisa.

Alisema ujio wa aina yeyote unahitaji maandalizi. “Tunapopata ugeni au  ujio wa kiongozi tunafanya maandalizi, na aina ya maandalizi inaamuliwa na mgeni husika alisema” Tunapopata ujio wa viongozi au mgeni tunafanya maandalizi makubwa na  leo tunaambiwa Bwana Yesu analijia Kanisa lake, huyu Bwana Yesu  ni Mwenye nguvu, hivyo ugeni wake ni mkuu kuliko ugeni wa aina yeyote.

“Ujio huu sii wa kawaida, ni ujio mkubwa kwa hiyo maandalizi tunayopaswa kufanya yanapaswa kuwa makunmbwa” alisema Mchungaji Msanya.


Anasema ugeni wowote hua  na ratiba, lakini ugeni huu wa Bwana wa Mabwana hauna ratiba.
Maandalizi ya kumpokea huyu anayekuja yana upekee wake maana hatujapewa muda wala saa atakayokuja kulinyakua Kanisa lake.
Neno la Mungu linatuelekeza jinsi gani ya kufanya maandalizi kwa maana hatuna ratiba ni lini wala saa gani Bwana atalijia Kanisa.

Bwana wa Kanisa kwa utaratibu wake hajatupa ratiba, na ametuambia kesheni maana hamjui ni siku gani wala saa atakayokuja
Anasema Kukesha ni kuwa macho au kukaa macho usiku kucha kwa shughuli maalum; Yesu anapotuambia tukeshe si maana hii ya kuwa macho wakati wote kiroo, kwa kukusanyika na kumwabudu Mungu.

Njiaa Moja wapo ya kukesha ni kukusanyika kama tulivyokusanyika leo hapa ibadani.
Kahimiza watu wote kukusanyika na kumwabudu Mungu katika Ibada Kanisani na kwenye jumuiya zetu. Ibada zinatusaidia katika maandalizi ya kumngojea Yesu alisistiza.


Namna nyingine ya kukesha ni kwa njia ya sala, Biblia inaseama Kesheni Muombe msije mkaingia majaribuni. Vishawishi ni vingi lakini kwa njia ya sala mnaweza kuwa macho kiroho na Bwana atakapokuja tutakuwa katika hali ya kumpokea. “Mwisho wa Mambo yote umekaribia iweni na akili na kukesha katika sala” alisema.
Anasema njia nyingine muhimu ya kukesha ni kujifunza neno la Mungu. Anasema Biblia inasema neno lako la Mungu ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia yangu. Neno la Mungu linaonya, linaelekeza na kwanjia ya neno la Mungu tunafundishwa.

Mhe.Baba  Askofu Dkt. Fredrick Shoo katika salam zake aliwaasa Wakristo na jamii  kujiandaa kumpokea Yesu. Tusijiandae kumpokea Yesu katika mavazi, chakula n.k, bali tuandae mioyo yetu kwa kuacha mambo maovu na kuwa na uhusiano mzuri  kati yetu sisi na Mungu.