Watoto wenye Ulemavu wa akili katika Sharika za Manispaa ya Moshi wanaotunzwa na kitengo cha Building a caring Community (BCC) cha KKKT Dayosisi ya Kaskazini wameshiriki michezo mbalimbali Julai 29, 2022 katika viwanja vya Uhuru Lutheran and Conference Centre.
Siku hiyo maalumu kwa ajili ya michezo hufanyika mara moja kila mwaka na hufadhiliwa na wahisani toka shirika la Mosaic International la Marekani linalojishughulisha na kuwahudumia watoto wenye ulemavu wa akili wakishirikiana na KKKT Dayosisi ya Kaskazini.
Michezo hiyo ni pamoja na mpira wa miguu, muziki na michezo mingine. Jumla ya takribani watoto 90 walishiriki.
Bulding a Caring Community BCC ni huduma inayoshughulika na watoto wenye ulemavu wa akili inayoshughulika na watoto waliopo nyumbani na wale waliopo kwenye vituo katika sharika 8 za manispaa ya Moshi. Katika sharika hizo kuna vituo ambayo vinawatunza watoto hao kuanzia asubuhi hadi jioni wanaporudi nyumbani.
BCC Ilianzishwa kutoa huduma hiyo kwa lengo la kuwasaidia katika matibabu, mazoezi ya mwili na pia kuwasaidia wazazi waweze kupata muda wa kufanya shughuli kutokana na kushindwa kufanya kazi wakiwa wanawahudumia watoto wao.
