Idara ya Elimu ya Kikristo ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini imeendesha semina ya kuwaongezea uwezo wainjilisti katika kufundisha elimu ya Kikristo, ikilenga kuboresha utoaji wa elimu hiyo katika shule za msingi na sharika.
Semina hiyo imefanyika Oktoba 14, 2026, katika Jimbo la Karatu na kuwashirikisha wainjilisti kutoka sharika 15 za jimbo hilo.
Miongoni mwa mada zilizojadiliwa ni umuhimu wa Elimu ya Kikristo katika karne ya 21, pamoja na maandalizi ya masomo ya elimu ya Kikristo na maadili kwa wanafunzi wa shule za msingi.
Semina hiyo imeongozwa na wakufunzi wawili, ambao ni Mchungaji Fadhili Kiwera kutoka Idara ya Elimu ya Kikristo katika Makao Makuu ya Dayosisi, na Mwinjilisti Ahimidiwe Lema.
Kupitia semina hiyo, Wainjilisti wanatarajiwa kuimarisha uwezo wao wa kufundisha vipindi vya dini mashuleni, kuendesha mafunzo ya kipaimara na kusimamia shughuli za Shule ya Jumapili katika Sharika zao.
