Jamii imetakiwa kubadilika na kuona umuhimu wa kuwalea watoto wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kuwapeleka katika vituo vya kuwasaidia kwani wanaweza kuleta mabadiliko katika jamii endapo wataelekezwa na kufundishwa.
Hayo yameelezwa na Md. Elirehema Kaaya mratibu wa kitengo cha Bulding a Caring Community-BCC kwenye maadhimisho ya siku ya watoto wenye mtindio wa ubongo Julai 14,2023 yaliyoandandaliwa na kitengo hicho kilichopo chini ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini.
Alisema kuwa kutokana na elimu wanayoitoa kwa jamii, wazazi na walezi wamekuwa na uelewa ambao umesaidia kuondokana na dhana ya kusema kwamba mtoto mlemavu hawezi kufanya jambo lolote lenye manufaa kwenye jamii.
Akiwa katika maadhimisho hayo afisa maendeleo ya jamii manisapaa ya Moshi Dankani Mgati amesema kuwa huduma ya BCC imekuwa Mkombozi katika jamii kwani imekuwa ikiwaibua watoto waliofichwa katika jamii.
Mwenyekiti wa bodi ya BCC Wilfred Monyo Alisema Kanisa limeamua kuanzisha huduma inayotolewa na BCC kutokana na watoto hao kutokuwa na Tasisi ambayo ilikuwa ikiwasemea
Wazazi na walezi wa wtoto hao wamesema kuwa jamii imekuwa na uelewa mdogo kuhusiana na kuhudumia watoto wenye ulemavu na kutoa wito kwa wadau mbalimbali kuendelea kutoa elimu katika jamii ili waweze kuona umuhimu wa watoto hao
