Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini katika kikao Cha Halmashauri Kuu ya 241 limemchagua Eng. Zebhadia Ruben Moshi kuwa Katibu Mkuu. Kuchaguliwa kwake Kumefanyika baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu Bw. Authur Ndengerio Shoo kufariki.
Injinia Moshi alikuwa Mkurugenzi wa VETA Tanzania(Director General at Vocation Education and Training Authority)-VETA na baada ya kustaafu alijishughulisha na shughuli binafsi.
