KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI OFISI KUU IMEPOKEA WAGENI KUTOKA UJERUMANI

Katibu mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mhandisi Z.S Moshi amepokea wageni  kutoka Ujerumani walioambatana na wenyeji wao kutoka Jimbo la Kilimanjaro Kati.

Wageni hao ambao wamezuru Dayosisi ya Kaskazini kwa lengo la kuimarisha uhusiano uliopo pia wametembelea Idara na miradi mbalimbali ya Kanisa.

Ofisi kuu ya Dayosisi ya Kaskazini kupitia Ndugu, Donald Massawe imetoa wasilisho la Dayosisi kama ilivyo kawaida kwa wageni wanapowatembelea.

Aidha wageni hao wamefurahishwa na wasilisho hilo na kuipongeza Dayosisi ya Kaskazini kwa kazi kubwa wanayoifanya.