KKKT Dayosisi ya Kaskazini wapata heshima ya kuwa Mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Wadiakonia Duniani utakaofanyika mwezi Julai, 2025.
Juni 5, 2024 Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Diakonia Duniani (Diakonia World Executive Committee), walikutana kwenye Ofisi Kuu ya Dayosisi kupeana habari ya maendeleo ya maandalizi ya mkutano huo
Pichani ni Kamati ya Tanzania ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wadiakonia Duniani {Diakonia World} walipokutana na Kamati ya Utendaji ya Diakonia Duniani {Diakonia World Executive Committee} kuhabarishana juu ya maandalizi ya Mkutano wa Wadiakonia Duniani utakaofanyika Nchini Tanzania mwezi Julai, 2025 ambapo KKKT Dayosisi ya Kaskazini ndiye wenyeji wa Mkutano huo.