Konde Yatembelea Dayosisi ya Kaskazini

Jopo la Wachungaji 18 wa KKKT Dayosisi ya Konde Jimbo la Mbeya Magharibi wametembelea KKKT Dayosisi ya Kaskazini.

Katika ziara hiyo iliyoongozwa na Mkuu wa Jimbo la Mbeya Magharibi Mch. Lusajano Sanga ililenga kuimarisha ushirikiano wa Dayosisi hizi mbili pamoja na kujifunza mambo mbalimbali yanayofanyika katika Dayosisi ya Kaskazini.

Hata hivyo walipata fursa ya kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanyika katika Dayosisi ya Kaskazini kupitia wasilisho la jumla la shughuli zinazofanyika katika Dayosisi.

Wakati wa salamu Mkuu wa jimbo la Mbeya Magharibi Mch. Lusajano Sanga amesema wamejifunza mambo mengi na kuahidi kuyafanyia kazi watakaporejea.

“Tunafurahi kuwa hapa. Mkuu wa Dayosisi na Msaidizi wa Askofu wanajua tuko hapa Dayosisi ya Kaskazini. Wametuma salamu nyingi za upendo” Alisema Mch. Lusajano

Mch. Lusajano ametumia nafasi hiyo pia kuwashukuru wote kwa kuwaombea na kuwatia moyo wakati wa changamoto ya mgogoro katika Dayosisi ya Konde.

“Tunazidi kuelewa maana ya umoja wa KKKT, Asanteni sana kwa kutupokea, tumeona, tumesikia na tumejifunza mengi, Sasa ni wajibu wetu kuyatendendea kazi tuliyoyapata hapa” Alisema Mch. Lusajano.