Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) imefanya ibada ya maalumu ya madhimisho ya siku ya CCT mkoa wa Kilimanjaro tarehe 8 Mei, 2025. Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ni neno la Mungu kutoka katika kitabu cha Mithali 14:34 “Haki huinua taifa; bali dhambi ni aibu ya watu wowote” .
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Kilimanjaro, Askofu Charles Mjema alisema, siku ya CCT huadhimishwa kila mwezi wa tano na kilele chake huwa ni kila Jumapili ya mwisho ya mwezi Mei kila mwaka. Lengo la maadhimisho ya Siku ya CCT (CCT Day) ni kudumisha Umoja wa CCT na kuitegemeza CCT katika utoaji wa huduma za kitume na kijamii.
Aidha, Askofu Mjema alisema kuwa, kauli mbiu ya mwaka huu ni ujumbe kwa taifa na wanajamii wasikie juu ya haki. Kwamba haki isipotendeka hakuna amani.
“Jamii yeyote ambayo hakuna amani watu wake hawawezi kufanya chochote, angalia nchi ya Kongo mahali ambapo hakuna amani ni vita kila wakati”.