Raisi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Ethiopia Askofu Yonas Dibisa na Maaskofu wa Sinodi za Ethiopia wametembelea Ofisi kuu ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini Julai 13, 2021.
Ziara hiyo iliyowahusisha maaskofu 42 na baadhi ya maofisa wa Makao Makuu ya Kanisa la Ethiopia na Sinondi zake ililenga kujifunza mambo kadha wa kadha yanayofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania.
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Ethiopia ni mwanachama wa Shirikisho la Makanisa ya Kilutheri Duniani LWF ambapo Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ni Mwanachama.
Katika ziara hiyo walipata maelezo kukutoka Uchumi Commercial Bank (UCB), Chama cha Akiba na Mikopo cha KKKT Dayosisi ya Kaskazini-ELCT ND SACCOS Pamoja na Idara za Dayosisi ya Kaskazini.
Vituo vingine walivyotembelea kabla ya kurejea Arusha yalipo Makao Makuu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)ni pamoja na kituo cha Masista wa Ushirika wa Neema cha Dayosisi ya Kaskazini na Hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) na Radio Sauti ya Injili vya KKKT.
