MCH. MSANYA “KANISA LINA WAJIBU WA KUTOA ELIMU YA AFYA….

Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mch. Deogratius Msanya amesema kuwa, Kanisa lina wajibu wa kutoa elimu  ya afya ili kuhakikisha kuwa washarika wanajikinga na magonjwa mbalimbali hususani magonjwa yasiyo yakuambukiza.

Aliyasema hayo wakati akihitimisha maadhimisho ya wiki ya afya ya msingi, kidayosisi yaliyofanyika jimbo la Karatu Usharika wa Endalah Julai 14, 2024.

Alisema kuwa elimu ya afya inapotolewa kwa  washarika na jamii wataelewa umuhimu wa kutunza afya zao. Alisema waumini wanapokuwa na afya nzuri wataweza kumtumikia Mungu.

Kwa upande wa Washarika walioshiriki katika siku hiyo wamesema kuwa elimu na vipimo walivyopata imewasaidia kugundua kuwa walikuwa wakiishi na magonjwa bila wao kutambua .

Katika kilele hicho, Washarika wa usharika wa Endalah na wasio washarika huo  wamejitokeza kwa wingi kupima afya zao na kupewa elimu ya afya , pamoja na umuhimu wa matumizi ya vyakula vya asili katika maisha wanayoishi.