Semina ya parish workers wa Kanisa la Kiiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini imefanyika Oktoba 27 hadi 30 katika kituo cha wanawake Angaza Sanya Juu Semina hiyo kuwaimarisha watumishi hao katika huduma.
Akifundisha mada kuhusu wito, Mhe. msaidizi wa Askofu Mchungaji Deogratius Msanya alisema tunapaswa kujua uzito na kutambua aliyekuita ni Mungu pekee.
Anasema ukijua aliyekuita na ukijua mamlaka yake utatambua upekee wa wito na uzito wake “Mungu ametuita na hajatuita kama kundi Bali Kila mtu kamwita kwa jina lake atumike” alisema Mchungaji Msanya
Pia alifundisha mwenendo unaostahili wito, ambapo alitaja kuwa moja wapo ni kula chakula, yaani kujifunza neno la Mungu. Kasema kubakia katika wito kunategemea sana jinsi unavyokula chakula (Neno). Kama hatuna neno la Mungu kwa ajili yetu ni rahisi sana kuacha wito, kuzolewa na majaribu, vikwazo na kupelekwa huku na huko kufuata mafundisho ya uwongo.
Kadhalika alisema mwenendo unaostahili ni kunywa maji na kupumua vyakutosha. Anasema maji ni sala na maombi, Yesu alikuwa muombaji wakati wote, bila maombi ni ngumu kubaki katika wito.
Semina hiyo iliandaliwa na Idara ya Wanawake na Watoto ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini inayoongozwa na Mchungaji Faustine Kahwa.