Askofu Dkt. Fredrick Shoo amekutana na walimu wa shule mbalimbali za kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini tarehe 01/02/2025 kwenye ukumbi wa Uhuru Lutheran Hotel.
Kwenye mkutano huo wa Askofu na walimu, Askofu Dkt. Shoo amezitunuku tuzo, shule zilizofanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani, tuzo zingine zilizotolewa ni tuzo za mjongeo chanya.
Aliongeza kuwa, japo zipo changamoto mbalimbali katika shule za kanisa, bado walimu hao wameendelea kufanya kazi kwa moyo wa kujituma na kwa uaminifu.
Juhudi na nidhamu ya hali ya juu inahitajika ili kufanikiwa alisema Askofu Shoo. Kwa wale waliofanikiwa aliwaasa kuendeleza mafanikio hayo na kwa zile shule ambazo hazikufanikiwa, aliwaasa kufanya vizuri, kwa kuwa bado wana nafasi ya kufanya hivyo.