Huduma ya Udiakonia-Injili kwa njia ya maneno na matendo ya huruma yanayoongozwa katika upendo wa Yesu Kristo kwa wahitaji. Kupitia huduma hii Wajane, Yatima, Wagane na waishio katika mazingira magumu ni miongoni wa wahitaji maalumu waliojengewa nyumba bora na za kisasa ambazo awali nyumba zao zilikuwa zimeharibika vibaya na nyingine kuanguka kabisa.