UZINDUZI WA KITUO CHA MAFUNZO KWA WATOTO WENYE ULEMAVU WA AKILI – BCC

Katibu wa Idara ya Udiakonia na Mratibu wa Kitengo cha Building a Caring Community (BCC), Mdiakonia Elirehema Kaaya, amesema kuwa uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mafunzo pamoja na miradi ya kiuchumi ni hatua muhimu ya kurejesha utu na kujenga matumaini mapya kwa watoto na vijana wenye ulemavu wa akili.

Uzinduzi huo, uliofanyika tarehe 22 Januari 2026, uliongozwa na Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo, na unalisisha uzinduzi wa jengo la kituo pamoja na miradi ya mashine ya kusaga nafaka, kilimo cha mboga mboga, ufugaji wa nguruwe na kuku.

Kwa mujibu wa Mdiakonia Elirehema Kaaya, miradi hiyo imelenga kuwajengea vijana hao ujuzi wa maisha na kuwawezesha kujitegemea kiuchumi, hivyo kuishi kwa heshima na kujiona kuwa sehemu kamili ya jamii.

Ameeleza kuwa ujenzi wa jengo la kituo hicho umegharimu jumla ya shilingi Milioni 60 za Kitanzania

Aidha, ametoa wito kwa majirani wa eneo hilo wakiongozwa na Usharika wa Shiri kushirikiana katika kuhudumia kundi hili maalumu