Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo amewataka viongozi wa dini mbalimbali kuungangana kwa pamoja na kusimamia na kupinga vitendo wanavyofanyiwa watoto wadogo pamoja na kusimamia misingi ya maadili katika ngazi zote.
Askofu Shoo ambaye ni mwenyekiti wa dini mbalimbali ( interfaith )mkoa wa Kilimanjaro ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa viongozi wa Dini mbalimbali interfaitth iliyofanyika Mkoani Kilinanjaro Aprili 12, 2023.
Aidha amesema kuwa amesema kuwa wanaowafanyia watoto vitendo vya kikatili sio wanafanya kwa matakwaa Yao baali wengine wanafanya kutokana na Imani za Kishirikina.
Akiwa mgeni Rasmi katika Mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdini Babu, Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro Tikson Nzunda amesema kuwa Serikali ipo sambamba na wao katika kukemea na kupinga ukatili wanofanyiwa watoto wadogo.
Mwakilishi wa mkurugenzi mkazi wa shirika la Norwegian Church Aid ( NCA) Berte Marie wadhamini wa Miradi mbalimbali inayotekelezwa kupitia KKKT Dayosisi ya Kaskazini amesema wataendelea kushirikiana na viongozi wa Dini mbalimbali Katika kutetea haki , kupinga unyanyasaji, ukatili na kutunza uumbaji wa Mungu
Hata hivyo akizungumza katika Mkutano huo, Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro Askofu Stanley Hotay amesema kuwa si vyema mashirika ya kutetea haki za binadamu kuwa kimya kaatika kipindi hiki cha kupingana na maswala ya Ukatili.
