Askofu Dkt. Shoo Aongoza Harambee huko Sinai

Mkuu wa Kanisa, Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo, ameongoza ibada ya Harambee ya Ujenzi wa Nyumba ya Ibada Mtaa wa Majengo Usharika wa Sinai Dayosisi ya Meru tarehe 26 Septemba 2021.

Akihubiri Neno la Mungu toka Yoshua 24:14-15, amewataka washarika kuchagua kumtumikia BWANA kwa furaha; kwani Yeye ni Mungu aliyetuumba na tu mali yake.

Mhe. Askofu Dkt. Elias Kitoi Nasari, Mkuu wa Dayosisi ya Meru, alisoma Neno la Mungu toka Kutoka 23:25-26 kwamba imetupasa kumtumikia Mungu.

Washarika walimpokea Mkuu wa Kanisa kwa shangwe na Laigwanani Yese Kamundulu Lesimanga Laiza alimsimika Mhe. Askofu Dkt. Frederick Onael Shoo kuwa Laigwanani. Katika Harambee hiyo zaidi ya 10M zilipatikana.