Mkuu wa Jimbo la Kilimanjaro Kati KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mch. Javason Mrema ameeleza jinsi uinjilishaji kwa njia ya pikipiki utakavyokuwa na manufaa.
Mch. Mrema ameeleza hayo wakati akiongea na Umoja Daima Media kwenye Usharika wa Ngorika C uliopo KKKT Dayosisi ya Kaskazini Jimbo la Kilimanjaro Kati ambapo waliwapokea waendesha pikipiki kutoka Ujerumani waliofika kwa ajili ya kuhamasisha uinjilishaji kwa njia ya pikipiki
Waendesha bodaboda wa usharika huo pia wameeleza jinsi walivyoelimika na namna watavyokwenda kufanyia kazi aina hii ya uinjilisti kwa njia ya pikipiki ikiwa ni pamoja na kuwahubiria abiria wao na boda boda wenzao habari za Yesu

