Askofu Dkt. Shoo awataka viongozi wa Dini Kupinga Ukatili kwa Watoto

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Askofu  Dkt. Fredrick Onael Shoo amewataka  viongozi wa dini  mbalimbali kuungangana kwa pamoja na kusimamia  na kupinga vitendo wanavyofanyiwa watoto  wadogo pamoja na kusimamia misingi ya maadili katika ngazi zote.

Askofu Shoo ambaye ni mwenyekiti wa dini mbalimbali ( interfaith  )mkoa wa Kilimanjaro  ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa viongozi wa Dini mbalimbali interfaitth iliyofanyika Mkoani  Kilinanjaro Aprili 12, 2023.

Aidha amesema kuwa amesema kuwa wanaowafanyia watoto vitendo vya kikatili sio wanafanya kwa matakwaa Yao baali wengine wanafanya kutokana na Imani za Kishirikina.

Akiwa  mgeni Rasmi katika Mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdini Babu, Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro  Tikson Nzunda amesema kuwa Serikali ipo sambamba na wao katika kukemea na kupinga ukatili wanofanyiwa watoto wadogo.

Mwakilishi wa mkurugenzi mkazi wa shirika la Norwegian  Church Aid ( NCA) Berte Marie wadhamini wa Miradi mbalimbali inayotekelezwa kupitia KKKT Dayosisi ya Kaskazini amesema wataendelea kushirikiana na viongozi wa Dini mbalimbali Katika kutetea haki , kupinga unyanyasaji, ukatili na kutunza uumbaji wa Mungu

Hata hivyo akizungumza   katika Mkutano huo,  Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi  ya Mount Kilimanjaro Askofu Stanley  Hotay amesema kuwa si vyema mashirika ya kutetea haki za binadamu kuwa kimya kaatika kipindi hiki cha kupingana na maswala ya Ukatili.

Mkutano wa Viongozi wa Dini mbalimbali Mkoani Kilimanjaro