Askofu Shoo Aongoza Ibada Engarenairobi, Azindua Nyumba za Ibada na Kuweka Jiwe la Pembe

Mkuu wa Kanisa na Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo Jumapili ya Julai 17, 2022 ameongoza Ibada katika Usharika wa Ngarenairobi Jimbo la Siha. Katika ibada hiyo kwa nyakati tofauti Baba Askofu alizindua nyumba ya Ibada ya watoto wa shule ya  Jumapili na ofisi ya Usharika wa Engarenairobi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 49

Pia alizidua Kanisa la Mtaa wa Matadi lenye thamani ya shilingi milioni 100 na kuweka jiwe la msingi jengo la shule ya Jumapili litakalogharimu shilingi milioni 35. Katika kuhakisha jengo hilo la watoto linakamilika Baba Askofu Dkt. Shoo aliongoza harambee ambayo walikusanya zaidi ya shilingi milioni 16 taslimu pamoja na ahadi.

Baba Askofu Dkt. Shoo amewashukuru washarika wa Usharika wa Engarenairobi kwa kutambua umuhimu wa kuwepo kwa nyumba ya ibada ya watoto. “Mmefanya jambo la maana na la msingi sana kuandaa maahali ambapo watoto watakaa na kujifunza msingi wa neno la Mungu kama neno linavyosema mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee” Alisema Dkt. Shoo.

Baba Askofu Dkt. Shoo mwenye fimbo kwenye picha ya pamoja na watoto mara baada ya ufunguzi wa nyumba ya ibada ya watoto wa Shule ya Jumapili Usharika wa Engarenairobi Julai 17, 2022.