Askofu Shoo aongoza ibada yenye matukio matatu Uswaa

Mch. Walter Kundadede Kimaro Astaafu.

Mhe. Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo, Mkuu wa KKKT na Dayosisi ya Kaskazini, tarehe 7.11.2021 amengoza Ibada yenye matukio mbalimbali katika Usharika wa Uswaa Jimbo la Hai.

Kwanza alizindua na kuweka wakfu Nyumba ya Sala Betheli Mtaa wa Mangalo ambapo Mhe. Askofu Dkt. Erasto Kweka, aliwaasa wakristo kutumia Nyumba ya Sala kukutana na Mungu na kupokea Baraka zake. Pia sio ruhusa klabu za pombe kujengwa karibu ya Nyumba ya Sala au ya Mchungaji.

Pili alizindua Nyumba ya Sala Hosiana Mtaa wa Kekura Sinde.

Tatu alizindua Ujenzi wa Madarasa na Ofisi ya Uswaa English Medium Academy.

Nne alizindua Choo cha kisasa cha Usharika.

Tano alizindua Zahanati ambayo inalenga kuwa Kituo cha Afya.

Sita alimwingiza kazini P/W Eliasimba Tarimo.

Saba alimstaafisha kwa heshima Mch. Walter Kundadede Kimaro.

Askofu Dkt Fredrick Onael Shoo, akihubiri toka Mt. 5:9-10, alikaza kwamba, wapatanishi na watendao haki ni miongoni mwa Sifa za watakatifu bora na wenyeji wa Mbinguni.

Pamoja na Zawadi kutolea kwa Mchungaji aliyestaafu na Parishwoker aliyeingizwa kazini; kipekee washarika walimpa Mchungaji wao Kiongozi Calvin Kessy zawadi ya kumpongeza kwa bidii yake kubwa katika kuustawisha Usharika wa Uswaa Kiroho, Kiafya na Kielimu.

Ibadani Uraa