Dayosisi ya Kaskazini katika kutekeleza Maagizo ya Mkutano Mkuu wa 36 uliofanyika 18 Augusti 2020, kipekee yahusuyo Idara ya Mawasiliano, imeanzisha YouTube channel. Lengo kuu likiwa kuwahabarisha, kuwaelimisha na kuwaburudisha washarika na jamii kwa ujumla, hususan maswala ya yahusuyo misioni, elimu, afya, jinsia, tabianchi na uchumi.