Wachungaji wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini waliopo kazini washiriki faragha Usharika wa Shiri leo tarehe 5.11.2021.
Akifungua faragha hiyo, Mhe. Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo, amehimiza Wachungaji umuhimu wa kutulia kwa Bwana ili kupata nguvu za kuendelea kumtumikia Mungu kwa furaha. Marko 6:31a.
Mhe. Askofu Dkt. George Fihavango, Mkuu KKKT Dayosisi ya Kusini, aliwasilisha Mada kuhusu umuhimu wa kuwa faraghani ili kupokea nguvu ya kuwatuliza mioyo watu wa Mungu. Isaya 40:1-2
Naye Mch. Dkt. Eliona Kimaro aliwasilisha Mada ya pili kuhusu tunamtumikiaje Mungu asiyebadilika katika mazingira yanayobadilika. Waebrania 13:8; Zaburi 46:1-2.
Aidha, Gari la Baraka EMS na Jiko la Usharika wa Shiri vilizinduliwa.