Fuka: Ofisi ya Kisasa yafunguliwa Mtaa wa Lomakaa

Mkuu wa KKKT na Dayosisi ya Kaskazini Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo, amefungua ofisi ya Usharika wa Fuka mtaa wa Lomakaa na hosteli ya shule ya English Medium Fuka Aprili 10, 2023.

Akisoma risala, mwenyekiti wa majengo Usharika wa Fuka Bw. Andrea Msechu amesema, kazi ya ujenzi ilianza rasmi  mwaka 2010 na jiwe la msingi liliwekwa mwaka 2012.

Amesema Ofisi hiyo  hadi kukakamilika imegharimu kiasi cha shilingi milioni 175 na hosteli shilingi milioni 92 fedha ambazo zimetokana na michango ya  Washarika wa ndani, waliopo safarini pamoja na marafiki.

Neno la Mahubiri la  siku ya pili baada ya pasaka limetoka katika kitabu cha luka 24:36.

Awali aliwashukuru washarika wa Fuka kwa kushiriki katika kazi za Umoja ndani ya Dayosisi. Anasema miongoni mwa Sharika mbili zilizo kuwa wakwanza kukamilisha michango ya kazi za Umoja ni Usharika wa Fuka. Usharika mwingine alitaja kuwa ni Usharik wa Shiri. Pia aliwapongeza kwa kazi njema ya ofisi na hosteli.

Katika mahubiri yake yenye Kichwa cha somo tembea na Kristo aliyefufuka alisema Wakristo hawana sababu ya kuwa na  mashaka ya wapi tutakuwepo baada ya maisha ya hapa duniani maana ufufuo upo kama Yesu alivyokufa na kufufuka.

Anasema Yesu amejidhihirisha kwa wanafunzi na mitume kuwa amefufuka maana kulikuwepo na Mashaka ya kutokuamini kufufuka kwa Yesu.

Baba Askofu anasema tukumbushane kuondoa uoga na hofu katika maisha haya kwa maana Kristo amefufuka kweli.

“Amini kweli kuwa huyu Bwana aliyefufuka ndiye atakaye nishindia na kunipigania katika maisha” Alisema Askofu.

Hofu na mashaka katika maisha kumefanya watu kufanya mambo ambayo hayampendezi Mungu. Hofu na mashaka iimetunyima kuthubutu kufanya mambo kama biashara, kuingia katika Masomo n.k.

Anasema kama alivyojidhihirisha kwa wanafunzi wake na kuwaondolea hofu wale wote wanaomwamini atawaondolea hofu. Tembea na Imani kuwa Yesu atakupigania dhidi ya maadui nao watashindwa.

Watu kwa kuwa na hofu na kutokuwa na imani kuwa Yesu atawapigania wamejikuta wakitafuta nguvu za ushirikina katika maisha yao

Wakristo tembeeni na Yesu awe kiongozi wenu maana yeye ni kweli na uzima na yeyote atakayemfuata hata potea kwenye giza.

Wakristo/ Watu wa Yesu hata kama kuna jambo linaloleta shida na giza nene Yesu analeta nuru na kutushindia. “Nasikia kina mama mnayumbayumba kwa manabii huku na kule, najua kinachowasumbua ni hofu na mashaka. Lakini nawambieni mwamini Yesu maana atawashindia taabu zenu:Alisema Askofu Dkt. Shoo.

Alihitimisha kwa kuwataka Waktisto kupokea wajibu wa kumshudia Yesu kwa wengine kwa upendo na matendo yao kwa kila mmoja kufanya yampasayo  kwa nafasi yake.

Baba Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo akifungua rasmi Ofisi ya Mtaa wa Loakaa kwa kukata utepe. Aliyeshika kipaza sauti ni Mkuu wa Jimbo la Siha Mch. Elisa Kileo