Harambee, Jiwe la pembe, Uzinduzi Nyumba ya Wageni vyafanyika Uduru

Mhe. Askofu Dkt. Solomon Masangwa, Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, ameongoza Ibada ya Kuweka Jiwe la Pembe, Uzinduzi na Harambee ya kukamilisha Ujenzi wa Nyumba ya Wageni Usharika wa Uduru Jimbo la Hai tarehe 3.10.2021.

Mgeni rasmi wa Harambee hiyo, Mhe. Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, aliwakilishwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul, Mbunge.

Wageni wengine waliokuwepo ni Wabunge: Mhe. Dkt. Maghembe, Mbunge wa Afrika Mashariki; Mhe. Priscus Tarimo, Mbunge wa Moshi Mjini; Mhe. Shally Raymond, Mbunge Viti Maalum na Mhe. Saashisha Mafue, Mbunge wa Hai, ambaye ni mzawa wa Uduru.

Katika Harambee takriban Tzs. 70 millioni zilipatikana.