Ibada ya Harambee Usharika wa Upperkitete

Ibada ya harambee ya ujenzi wa Kanisa Usharika wa Apperkitete wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Jimbo la Karatu imefanyika Desemba 5, 2021. Ibada iliongozwa na Mkuu wa KKKT na Dayosisi ya Kaskazini Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo akishirikiana na Mkuu wa Jimbo la Karatu Mch Barikiel Panga, Mch Faustine Kahwa Katibu wa Idara ya Wanawake na watoto Dayosisi, Mch. Joseph Darabe  na Mch Kiongozi wa Usharika Mch. Gudluck Kimaro


Akihubiri katika ibada hiyo Baba Askofu Dkt. Shoo amewataka wakristo kujiweka tayari katika kipibdi hiki cha majilio kwa maana hakika Yesu atarudi tena kwa mara ya pili. Anasema ahadi za Mungu tangu mwanzo ni za kweli hivyo pamoja na mambo mengi yanayotokea tujue yakuwa hakika Yesu atarudi kwa mara ya pili na hatarudi katika hali ya umaskini bali atarudi na malaka.

Kuhusu ugonjwa wa Corona, amesema katika kipibdi hiki cha ugonjwa wa Corona, tuendelee kumtegemea Mungu na kumwomba aendelee kutushindia huku tukifuata taadhari kama wanavyoelekeza wataalamu wa afya.


Baada ya Mahubiri Baba Askofu aliongoza harambee ambapo milioni Zaidi ya 27 zilipatikana ikiwa ni taslimu na ahadi. Jengo hadi kukamilika litagharimu milioni 850.