Jubilii miaka 50 KCMC, Askofu Shoo amkumbusha Rais Samia kutibu mioyo iliyojeruhika

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ambaye ndiye Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini na mwenyekiti wa CCT Askofu Dkt. Fredrik Onael Shoo amemkumbusha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Samia Suluhu Hasani hotuba yake ya Kwanza alipoingia Madrakani na kuahii kutibu majeraha ya Watanzania.

Akizungumza katika ibada ya kuadhimisha miaka 50 ya hospitali ya rufaa ya KCM Mjini Moshi Oktoba 16, 2021, alisema Raisi Samia amegusa mioyo ya Watanzania na tumeona kweli ukigusa mioyo ya Watanzania. Napenda kukuhakikishia wewe ukiwa kama mama, kama Rais tunakupenda na Mungu akusaidie akuwezeshe usimame katika nafasi yako.

“Nina uhakika Mungu ataendelea kukutumia na uwe tayari kutumika ili watu wa Tanzania wawe na afya njema na pale Watanzania wamejeruhika kwa sababu moja au nyingine, mama wewe umruhuisu Mungu akufanye chombo cha kuwaponya watu majeraha yao”Alisema Askofu Dkt. Shoo.

Alisema kazi yao kubwa kama viongozi wa duini ni kuzidi kuliombea taifa na kuwaombea wanaotoa huduma katika vituo vya afya.

Naye Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasan katika hotuba yake alisema ataendelea kuhudumia Watanzania Jinsi na Kadri Mungu atakavyomwezesha. “Nitaendelea kuwatazama Watanzania kwa jicho la huruma kama jicho langu “ Alisema Rais Samia.

Katika Jubilee hiyo Rais Samia aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la mionzi na kuwekwa wakfu na Askofu Dkt. Fredrick Shoo. Pia alizindua kitabu cha Mpango na utekelezaji wa maadhimisho ya Jubilii ya Miaka 50 ya Hospitali ya KCMC.

Mkurugenzi  wa Hospitali ya KCMC Prof. Giliad Asenga alisema hospitali hiyo ilianzishwa mwaka 1971 ikiwa na vitanda takribani 300 na kufikia miaka 50 sasa inauwezo wa kupokea wagonjwa wa kulazwa zaidi ya 600.