Kanisa na Mazingira

Mkuu wa KKKT na Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo amekuwa mstari wa mbele katika jitihada za utunzaji na uhifadhi wa mazingira toka mwaka 1996. Hii inadhihirishwa na jitihada kadha wa kadha ambapo moja wapo ni kuwapo kwa siku ya Askofu na mazingira ambayo hufanyika kila mwezi Aprili.

Mwaka huu katika kuadhimisha siku ya Mazingira Baba Askofu aliongoza zoezi la upandaji miti ya asili zaidi ya 1000 katika shamba la vijana wa Dayosisi lenye ukubwa wa takribani hekari 50 lililopo Kyomu kata ya Kahe Magharibi Machi 21, 2021.

Akizindua zoezi hilo la upandaji miti Baba Askofu Shoo ametoa wito kwa Kanisa na jamii kwa ujumla kujiingiza kikamilifu katika utunzaji na uhifadhi wa mazingira ili kulinda uumbaji wa Mungu.

Mkuu wa KKKT na Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Dkt. Fredrick Onael Shoo akiotesha mti.