Karatu: PW Mallomba Astaafu, Katibu Aingizwa Kazini

Jumapili ya Desemba 12, 2021 Parish worker wa Jimbo la Karatu Bibi. Anna Mallomba alistaafishwa kwa heshima baada ya kutumika katika Jimbo la Karatu kwa miaka 46 kama Parish worker, Karani, Mtunza Hazina na Kaimu Katibu Mkuu wa Jimbo. Pia Katibu wa Jimbo Mwinjilisti Manase Paulo Pununta aliingizwa kazini rasmi.

Ibada hiyo iliyofanyika katika Usharika wa Karatu Mjini  iliongozwa na Mkuu wa Kanisa na Dayosisi ya Kaskazini Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo, akishirikiana na Msaidizi wa Askofu Mch. Deogratius Msanya, Mkuu wa Jimbo Mch Barikiel Panga, Mch Faustine Kahwa Katibu Idara ya Wanawake na watoto Dayosisi na  Mch kiongozi wa Usharika Mch. Emmanuel Kimaro.

Neno la Mahubiri lilitoka katika kitabu Cha Mathayo 3:5-12 lililohubiriwa na Mhe. Msaidizi wa Askofu Mch. Deogratius Msanya. Mch. Msanya alisema tunapojiandaa na kumbukizi ya kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye alimkomboa mwanadamu toka kwenye utumwa wa dhambi alisema tunapaswa kuweka nguvu kubwa katika kujianda kumpokea atakapokuja mara ya pili kulichukua Kanisa lake.

“Wakristo wengi tunafanya maandalizi kwa nguvu kubwa kwa kumbukizi ya ujio wake wa mara ya kwanza kuliko tunapojianda kumpokea atakapokuja mara ya pili kulinyakua Kanisa, tunatoa uzito kidogo Sana juu ya kujiandaa kwa ujio wake wa mara ya pili”

Anasema ujumbe wa leo tunaambiwa itengenezeni njia ya bwana kwa kufanya toba ya kweli.
Maandalizi tunayofanya kwa njia ya toba yanatusukuma kila mmoja kutafakari maisha yake, kugeuka kutoka katika maisha ya dhambi na kuishi maisha yenye usafi.

Itikio la Parish worker Mallomba
Katika neno la itikio la kukubali kustaafu Parish Worker Anna Malumbo alisema anakila sababu ya kumtukuza na kumshukuru Mungu kwa Neema na huruma hata kumwita amtumikie kwa Mika 46

“Sifa utukufu na heshima zimrudie Mungu mwenyewe” Alisema Mallomba. Anasema Mungu anemtendea mema na familia yake katika utumishi wake hadi kufikia siku ya kustaafu.


Katibu wa Jimbo la Karatu Manase Paulo akiingizwa Kazini