Katibu Mkuu Dk, atembelea Idara ya Mawasiliano

Katibu Mkuu mpya wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Eng. Zebhadia Moshi ametembelea ofisi ya Idara ya Mawasiliano ya Dayosisi Februari 16,2022 kufahamiana na watumishi na shughuli zinazofanywa na Idara. Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara alizofanya katika Idara nyingine na zitaendelea kwa Vituo vya KKKT Dayosisi ya Kaskazini.

Eng. Zebhadia  Ruben Moshi alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika kikao cha Halmashauri Kuu ya 241 kilichofanyia Disemba 7, 2021 Uhuru Hotel and Conference Centre.