Katibu Mkuu Msaidizi atembelea Bethilehemu

Katibu Mkuu Msaidizi na Mtunzahazina wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini CPA Munguatosha Makyao ametembelea usharika wa Kia mtaa Bethilehemu April 3, 2022. CPA Makyao aliongozana na mgeni kutoka Ujerumani Mch Harald ambaye ana mahusiano ya kirafiki na mtaa wa Bethilehemu na wanajamii wa Malula.

Bethilehemu ni kati ya mitaa 15 ya usharika wa Kia ambao ni miongoni mwa sharika za misioni za KKKT Dayosisi ya Kaskazini. Wengi wa wakazi wa eneo hili ni jamii ya kimasai na shughuli yao kubwa ni ufugaji.

Mchungaji Harald akiwasalimu washarika wa Bethilehemu alisema amefurahi kuwaona tena ndugu zake  wa Bethilehemu. Anasema anawatambua kama kaka na dada “Sisi sote ni watoto wa baba mmoja ambaye ni Mungu wa mbinguni.” Alisema Mchungaji Harald.

Kahimiza kuhusu kupendana kama Yesu alivyotuambia  amri kuu ninayowaachia ni upendo. “Tupendane sisi kwa sisi, ukimpenda mwenzako utamjali, utamuhudumia na kumthamini, tukipendana hutuwezi kufanyiana ubaya.”Alizumgumza Mchungaji Harald

Alisema watu wote tunapaswa kupendana na kusaidiana bila kujali unatokea wapi, una rangi gani, kabila na dini gani.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Msaidizi na Mtunzahazina wa Dayosisi CPA Mkyao alimkaribisha na kumshukuru Mch. Harald kwa moyo wake wa upendo anaouonyesha kwa washarika wa mtaa wa Bethilehemu na jamii ya Malula Kia.