KIKAO NA VIONGOZI WA HOSPITALI ZA KKKT DK.

Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mch. Deogratius Msanya, amefungua kikao cha viongozi wa Dayosisi na Madaktari viongozi, Makatibu wa Hospitali, Wenyeviti na wenyeviti wasaidizi wa Bodi za Hospitali za Dayosisi Februari 10, 2023 katika ukumbi wa Uhuru Lutheran Hotel and Conference Centre uliopo Shanty Town Moshi. Akifungua kikao hicho, Msaidizi wa Askofu Mch. Deogratius Msanya aliwapongeza viongozi hao, kwa kazi wanayoifanya katika kuwatumikia watu wa Mungu. Alisema kikao hicho ni muhimu kwao kuweza kutafakari changamoto na ushindani uliopo katika kutoa huduma bora.Alisema kufuatia kikao hicho, wanapaswa kujiuliza kama kweli huduma wanayotoa ina kidhi na kama kweli inamtangaza na kumtukuza Mungu.“Katika kikao hiki tusiwe wasikilizaji pekee, tusikilize na kujadili kwa kina na uwazi mafanikio, changamoto na jinsi ya kuweza kutoa majibu ya nini kifanyike kuweza kutoa huduma bora itakayomtukuza Mungu”.Alisema Mch. Msanya.Mada zilizowasilishwa na kujadiliwa ni ya utawala (Governance) na uendeshaji (operation)

Watatu kushoto ni CPA Munguatosha J. Makyao Mtunzahazina na Katibu Mkuu Msaidizi wa KKKT DK, kwenye kikao cha Viongozi wa Hospitali za Dayosisi kilichofanyika Uhuru Lutheran Hotel& Conference Centre Februari 10, 2023. Wengine ni Makatibu wa Hospitali na Madaktari viongozi