KKKT Dayosisi ya Kaskazini imekuwa mwenyeji wa mkutano wa (LMC) Shirika la Kimisionari la Kilutheri ambao hufanyika kila mwaka. Mwaka huu mkutano huo unafanyika tarehe 01-04 Octoba, 2024 katika hoteli ya Uhuru iliyopo mjini Moshi- Kilimanjaro.
Katika Mkutano huo mada kuu ni “KUJENGA AMANI KATIKA DUNIA YENYE CHANGAMOTO NYINGI”
Mathayo 5:9.
Lutheran Mission Cooperation ni chombo cha pamoja cha uratibu wa ushirikiano kati ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania na washirika wake kutoka Ulaya na Amerika. Dayosisi 28 za KKKT, Makanisa na Mashirika 13 ya Kimisionari kutoka Finland, Sweden, Norway, Denmark, Ujerumani na Marekani ndio waliounda Ushirika wa Kimisheni wa Kilutheri ili kuratibu utendaji wao wa kazi kwa pamoja katika kueneza Injili ya Yesu Kristo, nchini Tanzania lakini pia nchi za Kaskazini.