Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzani na Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo, ameweka wakfu na kukabidhi gari mpya aina ya Land Cruiser kwa Kituo cha Mafunzo ya Udiakonia Faraja cha KKKT Dayosisi ya Kaskazini Oktoba 13, 2021 katika ofisi kuu za Dayosisi Moshi.
Gari hilo lenye thamani ya shilingi milioni za Kitanzania 69 limetolewa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Bavaria kupitia idara ya misioni (Mission one World) kwa jitihada za katibu wa Dawati Afrika na Tanzania Mdiakonia Claus Heim.
Baba Askofu Shoo aliwapongeza kwa kupata gari hilo na kuwaasa wakalitumie ipasavyo katika kuwahudumia watu kama kusududi lilivyo.