Machame: Juma la Baba Askofu na Vijana 2021

Juma la Baba Askofu na Vijana limefanyika Disemba 13 hadi 18 katika shule ya Sekondari ya Wasichana Machame (Machame Girls Secondary) Jimbo la Hai ulipo Usarika wa Nkwarungo. Mhe. Msaidizi wa Askofu Mch. Deogratius Msanya alifungua rasmi  Juma hilo Desemba 14, 2021 akimwakilisha Baba Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo. Neno Kuu lilitoka kitabu cha Mithali 28:20
Akifundisha neno kuu Mhe. msaidizi wa Askofu aliwataka vijana kuwa waaminifu. Anasema kwa sasa Vijana wengi wanapenda mafanikio ya haraka haraka jambo linaloasababisha kukosa uaminifu ambapo ni kinyume na mapenzi ya mungu” Kukosa uaminifu sio picha nzuri, tunapaswa kuwa vijana wenye Sifa njema” Alisema Mchungaji Msanya”

Biblia inatuambia Mungu wetu tabia yake ni uaminifu nasi wakristo tunapaswa kuonyesha kuwa na tabia ya Mungu ya kuwa waaminifu  Ufunuo 3:14.

Vijana wote walioshiriki walifundishwa kuhusu Neno Kuu Mithali.28:20 na mada za Ujasiriamali, Maadili ya Kijana Mkristo, Urafiki Uchumba hadi Ndoa, uwakili wa Wakati, Utumishi wa Kijana katika Kanisa la Mungu.

Mada nyingine ni  Ufugaji wa Kuku, Mpango uitwao Fikia Maisha Chaguo ni lako kutoka Chama cha Biblia ambapo walipewa  kitabu kiitwachwo Fikia Maisha na kuwekewa mpango wa jinsi ya kukisoma na kukielewa .