Mahafali Machame:Wauguzi, Matabibu 105 wahitimu Machame

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  na Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ambaye pia ndiye mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo amewatunuku vyeti wahitimu 105 wa Uuguzi na Utabibu katika Taasisi ya Mafunzo ya Afya Machame Septemba 11, 2021.

Baba Askofu Shoo aliwatunuku wahitimu hao vyeti vyao baada ya kufuzu katika fani ya Uuguzi na Utabibu inayotolewa chuoni hapo. Kati ya wahitimu hao 105, wahitimu 22 walifuzu katika fani ya Uuguzi na 83 katika fani ya Utabibu.

Akihutubu katika mahafali hayo Baba Askofu Shoo aliwataka wahitimu hao kutumika kwa uweledi na kuzingatia maadili mema “Huu ni wito natoa kwenu, mkienda huko mkatumike kwa upendo, bidii na uamnifu, taaluma pekee haitoshi bila kuzingatia suala la utu”Alisema Askofu Shoo.

Aliwapongeza wahitimu hao, uongozi na Bodi kwa jitihada wanazofanya chuoni hapo ikiwa ni pamoja na kutatua suala la mfumo wa kupasha moto maji ya kuoga na mpango wa ujenzi wa hosteli ya wanaume.

Taasisi ya mafunzo ya Afya Machame ilipo Hospitali ya Kilutheri Machame, inamilikiwa na KKKT Dayosisi ya Kaskazini.

Baba Askofu Shoo wapili kushoto kwenye picha ya pamoja mahafali ya 4 Machame