MCH. DKT. ROSE MATERU ASTAAFU KWA HESHIMA

Mkuu wa KKKT na Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo, amemstaafisha kwa heshima Mch. Dkt. Rose H. Materu katika Usharika wa Tela, Jimbo la Kilimanjaro Kati tarehe 08.08.2021.

Dkt. Rose ni miongoni mwa Watheolojia Wanawake Wawili wa kwanza katika KKKT na Mtheologia mwanamke wa kwanza Dayosisi ya Kaskazini. Pia ni miongoni mwa Wachungaji Wanawake wa Kwanza kubarikiwa katika Dayosisi ya Kaskazini.

Baba Askofu Dkt. F. Shoo akimstaafisha Mch. Dkt. Rose Materu mwenye barakoa nyeusi Jumapili ya tarehe 08 Agosti, 2021.