Mitaa 8 yafunguliwa Kia

Mkuu wa KKKT na Dayosisi ya Kaskazini Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo, akishirikiana na Askofu wa Kanisa la Kinjili la Kilutheri Bavaria Nchini Ujerumani Askofu Dkt. Strohn Bedford Heinrich wameweka mawe ya pembe na kuzindua jumla ya mitaa 8 ya Usharika wa Kia Jimbo la Hai la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mwezi Oktoba 2022.

Mitaa iliyozinduliwa na mingine kuwekwa jiwe la pembe ni pamoja na Sanya Station, Sinai, Bethel, Bethlehemu, Sayuni, Kaanani, Yerusalem na mtaa wa Mtakuja.

Katika uzinduzi huo, Mkuu wa Kanisa la kiinjili la kilutheri Bavaria Nchini Ujerumani Dkt. Strohn Bedford Heinrich amewataka waumini Wakristo kuwa na Upendo na kuondoa chuki ndani ya mioyo yao wakiishi maisha ya Kama kaka dada ndani ya Kristo.

Amesema kuwa endapo kila mmoja ataambatana na mwenzake kama kaka na dada bila kujali kabila, rangi au tofauti yeyote, italeta tumaini kubwa kwenye hii Dunia ya leo.

“Kulikuwa na kongamano kubwa huko Ujerumani linalohusu upendo na amani na ndio ulikuwa Msingi wa kutaniko hilo. Amesema katika kongamano hilo jambo kuuu lililojadiliwa lilikuwa Upendo wa Mungu unaolekeza kupatana pamoja na kuhimiza upendano hususani watu wa ulaya kutokana na vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine.

Kongamano hilo lilifanyika kuanzia Agosti 29 hadi Septemba 8, 2022.  Mkutano huo hufanyika mara moja takribani kila baada ya miaka 7 na  Makanisa Wanachama 352 yenye waumini zaidi ya milioni 580 kutoka madhehebu ya Anglican, Lutheran, Methodist, Baptist, Katoliki na mengine katika nchi 120.

Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kia Timoth Meena amesema kuwa, katika ukanda huo wa tambarare kwa sasa  wanakabiliwa na changamoto ya waumini wengi kutohudhuria ibada kutokana na jamii ya waamaasai kufanya vikao vya kimila siku za ibada.

Amesema kuwa wamefanya jitihada nyingi za kuwarudisha kwa kuwapa mafundisho lakini bado wamekuwa hawazingatii mafundisho hayo.

Sambamba na hayo amesema kuwa wanakabiliwa na uwezo mdogo wa kutunza watumishi kutokana na na Hali ya uchumi na kusema hali ya ukame wa muda mrefu pamoja na kuishikuru dayosisi kwa kuwapatia msaada wa chakula pindi wanapopatwa Neema ya chakula.

Nao baadhi ya wakristo akiwemo Daudi Ezekiel amesema kuwa kuzinduliwa kwa mitaa hiyo pamoja na ujenzi unaoendelea kwa baadhi ya makanisa itasaidia Wakristo kuhudhuria ibadani .