MITI ZAIDI YA 300 YAOTESHWA KKKT USHARIKA WA NKWARUNGO

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Usharika wa Nkwarungo kwa kuongozwa na Mchungaji kiongozi wa Usharika  huo, wamepanda miti zaidi ya mia tatu huku wakishirikiana  na  wanafunzi wa darasa la kipaimara kama ilivyoagizwa na Mkuu wa  KKKT na Mkuu wa Dayosisi  ya Kaskazini Askofu Dr. Fredrick Shoo kuwa, kila mwanafunzi anayeanza darasa la kipaimara aoteshe miti kumi mpaka atakapomaliza .

Akizungumza katika zoezi hilo la upandaji miti mchungaji kiongozi wa Usharika wa Nkwarungo Mch. John Mbando amesema kuwa watahakikisha miti hiyo inatunzwa ili hiyo iweze kuwa salama.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa jimbo la Hai Mchungaji Biniell Mallyo , Mchungaji Solomon Masawe, mshauri wa miradi na maendeleo ya Jimbo la Hai  ameashauri sheria za Dayosisi kuzingatia uoteshwaji wa miti ya matunda ili kutunza uoto wa asili.

Akiwa katika zoezi hilo la upandaji wa miti, Diwani wa kata ya Machame Kaskazini Bw. Judica Joseph Munisi  amesema kuwa serikali ipo tayari kushirikiana na Kanisa katika kutunza miti ambayo imekuwa ikioteshwa na washarika.

Hata hivyo walioshiriki katika upandaji wa miti wamesema kuwa kila mwaka wanaotesha miti kwani wana matumizi mbalimbali yatokanayo na miti.

Wanafunzi wa darasa la Kipaimara wakiwa katika shughuli ya uoteshaji miti- KKKT Usharika wa Nkwarungo.