Mkurugezi TAMISEMI: Kongole KKKT kwa kuwahudumia Walemavu.

Mkurugenzi wa huduma za jamii ofisi ya Rais TAMISEMI, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu Bi. Amina Faki, amelipongeza Kanisa kwa jitihada kubwa inayoifanya ya kuwahudumia watoto wenye ulemavu wa akili pamoja na makundi  mbalimbali ya watu wenye uhitaji maalumu..

Bi. Faki ametoa pongezi hizo kwenye bonanza la michezo la watoto wenye ulemavu wa akili Julai 12, 2024 katika viwanja vya Hindu Mandal vilivyoko Moshi mkoani Kilimanjaro. Bonanza hilo limeandaliwa na kitengo cha BCC (Building a Caring Community)  cha KKKT Dayosisi ya Kaskazini kinachowadumia watoto na vijana wenye ulemavu wa akili.

Alisema bonanza hilo la watoto na vijana wenye ulemavu wa akili linaonyesha kuwa kunauwezekano wa kuwa na jamii jumuishi isiyo na ubaguzi kwa watu wenye uihitaji maalumu.

“Napongeza uongozi wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, watendaji wote wa BCC ndani ya Idara ya Udiakonia pamoja na wote tuliopo hapa maana tunatambua umuhimu wa michezo na tunatambua umuhimu wa kila mtoto kwa sababu mtoto anatakiwa kuthaminiwa, anatakiwa kusemewa, anatakiwa kusaidiwa….”

Hii inadhihirisha sote hapa tunaelewa umuhimu huo, lakini umuhimu huu tusiuelewa pekee yetu tuupeleke na kwa makundi mengine ili thamani na utu wa watoto wetu uendelee kutunzwa na kutekelezwa na kila mwana jami.” Alisema Bi. Faki.

Tamasha hilo limehudhuriwa na watu zaidi ya 250, ambapo watu wote kwa pamoja wamepata muda wa kucheza na watoto.