Mkutano Mkuu wa 37 wa Dayosisi Wafanyika

Mutano Mkuu wa 37 wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini umefanyika Agosti 11, 2022 katika viwanja vya  Lutheran Uhuru Hotel & Conference Center. Katika mkutano huo mkuu wa Dayosisi Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo aliwasilisha taari ya Dayosisi kisha kujadiliwa na maazimio kutolewa na wajumbe.

Katika Hotuba yake Baba Askofu Dkt. Shoo alitoa rai kwa jamii kuweka akiba ya chakula kidogo kilichopatika kufuatia ukame uliosababishwa na mabadiliko ya tabia Nchi.

Katika hotuba yake pia aliwataka viongozi wa dini kusimama imara na kufundisha kweli ya neno la Mungu kwani kwa sasa kumeibuka mafundisho potofu ambayo yanawayumbisha Wakristo wengi.

Anasema mafundisho mengi yanalenga kuwapeleka watu katika mafanikio na hata kuleta mafarakano baina ya watu na watu.

Kuhusu suala la Sensa Dkt. Shoo alisema kuelekea Agosti 23, 2022 kutakua na zoezi la kitaifa la Sensa. Amesema sensa ni msingi wa mipango ya maendeleo ya Taifa na ni wajibu wa Kirai.

“Dayosisi inatoa wito kwa Washarika wote na jamii kwa ujumla kuhimizana na kujitokeza kuhesabiwa kwa manufaa ya mtu binafsi, familia na Taifa kwa ujumla.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu katika salamu zake alilipongeza Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzani Dayosisi ya Kaskazini kwa kuiunga serikali katika huduma za kijamii ikiwemo Elimu, Afya nk. 

Mkutano Mkuu hufanyika kila baada ya miaka miwili na ni mahususi kwaajili ya kuweka mipanngo ya maendeleo ya Dayosisi pamoja na tathimini ya kipindi cha miaka miwili.

Baadhi ya wajumbe kwenye picha ya pamoja ya Mkutano Mkuu wa 37 wa Dayosisi ya Kaskazini Agosti 11, 2022