Mkutano Mkuu wa 41 E/A-Msingi Wafanyika Dk.

Mkutano Mkuu wa 41 wa kitengo cha  Elimu ya Afya ya Msingi Dayosisi ya Kaskazini umefanyika katika ofisi kuu ya Dayosisi Machi 31, 2022.

Kitengo cha Elimu ya Afya ya Msingi kipo chini ya Idara ya Afya ya Dayosisi, kilianzishwa kwa lengo la kuijengea uwezo jamii katika kujikinga dhidi ya maradhi kupitia elimu ya afya, upimaji wa afya, na elimu ya mazingira.

Katika ufunguzi Mwenyekiti wa Mkutano Mhe. Msaidizi wa Askofu Mch Deogratius Msanya alisoma neno la ufunguzi kutoka kitabu cha Isaya 58:8. Alisema ili kanisa na taifa liwe na maendeleo mazuri watu wake wanapaswa kuwa na afya nzuri.

“Utajiri mkubwa kwa taifa lolote ni kuwa na raia wenye afya nzuri, Winston Churchill waziri Mkuu wa Uingereza aliwahi kusema maneno hayo”Alisema Mch. Msanya.

Anasema katika jimbo, sharika na kanisa kwa ujumla kama wakristo hawana afya njema mipango na shughuli haziwezi kutekelezeka kwa ufanisi.

Alisema suala la afya bora ni la msingi na ndiyo sababu ya kuanzisha kitengo hichi Cha Elimu ya Afya ya Msingi.

Mch. Msanya alisema ni vyema kuwapatia watu maarifa ya kujikinga zaidi kuliko kusubiri watu kuugua na kuweka nguvu kwenye tiba. “Tuwekeze kwenye kinga  zaidi kuliko kwenye tiba na tiba ina gharama  kuliko kinga” Alisema Mch. Msanya.

Aidha Katoa wito kwa waratibu wa Afya katika ngazi zote kutoa Elimu ya Afya kwa jamii ili kuwa na watu wenye afya kwa ustawi wa kanisa na kaifa.

Katia hatua nyingine Mhe. Msaidizi wa Askofu alitoa zawadi ya alama ya Shukrani ya utumishi kama Mratibu wa Elimu ya Afya ya Msingi Ji,mbo la Kilimanjaro Kati Bibi.  Beatrece Risasi.